IDD Cheche,
Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka leo kwenye
mchezo wa kimataifa dhidi ya Triangle United wapo tayari kutoa burudani na kupata ushindi.
Leo Azam FC
inamenyana na Triangel United ya Zimbabwe kwenye mchezo wa Kwanza wa hatua ya
Kombe la Shirikisho kabla ya kurejeana nao kati ya Septemba 27-29 nchini
Zimbabwe.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa walitumia muda mwingi kuwafundisha wachezaji
kwa kutumia Cd za wapinzani wao jambo linalowapa matumaini kupata ushindi leo.
“ Tupo sawa na tumewaandaa wachezaji wetu kupata matokeo chanya ni wakati wetu wa
kufanya makubwa na tutawapa burudani mashabiki na kupata matokeo chanya.
“Tuliwatuma
watu kwao na kuwatazama namna ambavyo wanafanya na tumechukua Cd zao za kutosha ili tuweze
kuwatambua vema wapinzani wetu hatuna mashaka na kikosi chetu,” amesema Cheche.
Kwenye michezo tisa mabay Azam imecheza baada ya kupanda ligi mwaka 2008, haijawahi kupoteza hata mmoja zaidi ya utoa sare miwili na kushinda michezo saba.
0 COMMENTS:
Post a Comment