September 16, 2019


SALUM Mayanga, Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting jana aliionja joto ya jiwe mbele ya Tanzania Prisons kwa kunyooshwa kwa mabao 2-1 mchezo wa pili wa ligi ugenini.

Mchezo wa kwanza Ruvu Shooting ilijikusanyia pointi tatu ikiwa ugenini mbele ya Yanga uwanja wa Uhuru jambo lililompa hali ya kujiamini Mayanga ambaye alipania kutumia mbinu alizotumia kuimaliza Yanga kushinda jana uwanja wa Sokoine.

Mabao ya ushindi kwa upande wa Prisons ambao mchezo wa kwanza walilazimisha sare mbele ya Mbeya City yalipachikwa na Jumanne Elifadhil dakika ya 15 na Ismail Kada dakika ya 37.

Bao pekee la kufuta machozi kwa Ruvu Shooting lilifungwa na Said Dilunga dakika ya 25 kwa mkwaju wa penalti.

1 COMMENTS:

  1. Hivi vitimu vidogo vidogo kazi ni kukazana kwa timu kubwa baada ya hapo kwisha, mdebedooooo!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic