September 16, 2019


TEMMY Abraham, nyota wa Chelsea amezidi kukiwasha kwa washambuliaji ndani ya Ligi Kuu ya England kwa kuwa kinara wa utupiaji kwa sasa.

Hat-trick aliyotupia dhidi ya Wolves siku ya Jumamosi wakati Chelsea ikiibuka na ushindi wa mabao 5-2 imempandisha kwenye chati nyota huyo.

Alipachika mabao hayo dakika ya 34,41 na 55 huku lile la ufunguzi likifungwa na Fikayo Tomari dk ya 31 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Mason Mount dakika ya 90+6.

Licha ya Abraham kujifunga dakika ya 69 na Patrick Cutrone kuongeza bao la pili bado mambo yaliwanyookea Chelsea ambao wapo chini ya Frank Lampard.

Idadi hiyo inamfanya afikishe jumla ya mabao 7 kwa sasa akiwa amecheza jumla ya michezo mitano EPL akiwa sawa na Sergio Arguero nyuma ya Teemu Pukki ambaye ametupia jumla ya mabao sita.

Pukki akiwa Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita alifunga jumla ya mabao 29 na Abraham yeye alitupia jumla ya mabao 25.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic