IKIWA kwa
sasa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na Vodacom ipo mzunguko wa kwanza
tayari kuna rekodi za kibabe ambazo zimewekwa na timu tatu Bongo zikiongozwa na
Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi.
Timu hizo
ambazo ni Simba, Lipuli na Namungo zimecheza jumla ya michezo miwili na
kujikusanyia jumla ya pointi sita kwa msimu huu jambo linaloongeza utamu wa
ligi.
Rekodi ya
kwanza ambayo timu hizi iliweka ni kushinda mechi za kwanza na majina ya
wachezaji wao kuibuka kwenye fainali ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi,
Simba iliwakilishwa na Meddie Kagere, Lipuli iliwakilishwa na Seif Karihe huku
Namungo wao wakiwakilishwa na Lukas Kikoti na mbabe wao akawa Kagere.
Pia kwenye
michezo yao ya pili zote zimefanikiwa kusepa na pointi tatu na kuwa miongoni
mwa timu ambazo zimeshinda mara mbili mfululizo kwa msimu huu mpya wa 2019/20.
Simba
ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar mabao 2-1 uwanja wa Uhuru, Namungo 2-0 dhidi ya
Singida United uwanja wa Majaliwa na Lipuli bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania
uwanja wa Isahmuyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment