JOHN Bocco, nahodha wa Simba, msimu uliopita uwanja wa Karume aliwanyanyua mashabiki wa
Simba kwa kufunga mabao 2 yaliyoipa pointi tatu Simba, hatakuwepo kesho jambo linalompasua kichwa, Kocha Mkuu, Patrick Aussems.
Simba
itashuka uwanjani kesho kumenyana na Biashara United mchezo wake wa nne wa ligi
bila Bocco ambaye anasumbuliwa na majeruhi ya goti aliyoyapata wakati Simba
ikicheza na Azam FC mchezo wa ngao ya Jamii.
Aussems amesema kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu ndani
ya kikosi chake ni Bocco ila atalazimika kuendelea na mapambano bila uwepo wake.
“Unapozungumzia
Simba kila mchezaji ana umuhimu wake hata Bocco pia ni muhimu hivyo kukosekana
kwake ni pigo kwa timu kiujumla, tuna michezo mingi muhimu na malengo yetu ni
kupata ushindi inanibidi niwape nafasi wengine,” amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment