YANGA KWENDA NA WAREMBO ZAMBIA KUPINDUA MEZA DHIDI YA ZESCO - VIDEO
Kamati ya hamasa ya Timu ya Yanga imewataka mashabiki na wapenzi wa Yanga kujumuika kwa umoja katika safari ya kuelekea nchini Zambia kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Zesco United utakaopigwa Septemba 28, mwaka huu Ndola nchini Zambia.
Akizungumza na waandishi wa mwenyekiti wa kamati ya hamasa ya Yanga Suma Mwaitenda amewashukuru mashabiki wa Yanga ambao walijitokeza katika katika mechi ya awali dhidi ya Zesco United kutokana na kuipa hamasa timu kwa kuishangilia huku akiwataka kuungana kwa pamoja kuelekea Zambia katika mchezo wa marudiano.
0 COMMENTS:
Post a Comment