SIBUSISO Vilakazi mshambuliaji wa timu ya Mamelodi Sundowns jana alitupia hat trick yake wakati timu yake ikiiua kwa jumla ya mabao 11-1 Cote d'Or kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Ijumaa usiku.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Lucas Moripe umeweka rekodi ya kukusanya mabao mengi kwa mechi zote za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mamelodi Sundowns inatinga kibabe hatua ya makundi ya Caf kwa kuiondoa Cote d'Or ya Seychelles kwa jumla ya mabao 16-1 kwani mchezo wa awali ilishinda mabao 5-0 hivyo itaendelea kuwa kwenye michuano ya kimataifa ila itashiriki Kombe la Shirikisho.








0 COMMENTS:
Post a Comment