September 18, 2019


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi wa kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Simba hii ni kutokana na uamuzi kutokamilika kuandikwa.

Kesi ambayo inawakabili waliokuwa viongozi wa Simba rais Evans Aveva na makamu wake Godfrey Nyange na  Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Zachariah Hans Pope, ilitarajiwa kutolewa uamuzi juzi Jumanne kama wanakesi ya kujibu au laa.

Tayari upande wa serikali ambao ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa walifunga ushahidi baada ya kuleta mashahidi wake 10 katika kesi hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kuwa uamuzi huo atautoa kesho Alhamisi ili kuhakikisha kesi hiyo inaenda kama ambavyo walikuwa wamepanga awali.

Hata hivyo uamuzi wa kesi hiyo ulishindwa kutolewa kutokana na kutokamilika katika uandikaji hii ni kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi. 

Simba alisema kesi hiyo itaendelea kesho Alhamisi ndipo ataweza kutoa uamuzi.

Ikumbukwe  mashitaka yao ni pamoja na inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic