Kikosi cha Simba jana kiliendelea na mazoezi yake kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Septemba 29 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba baada ya kutoka kwenye mapumziko ya siku mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazoezi ya timu hiyo, Kocha Mkuu, Patrick Aussems, alisema kuwa kuna baadhi ya wachezaji wake ambao hawapo kwenye mazoezi wakiwemo ambao wameitwa katika Timu ya Taifa ya Tanzania na wengine kuwa majeruhi akiwemo John Bocco pamoja na Meddie Kagere.
Aidha Kocha Aussems alisema kikosi chake kipo vizuri kwa mchezo wao dhidi ya Kagera kutokana na msimu uliopita kupoteza pointi sita dhidi ya timu hiyo huku Jonas Mkude na Miraji Athumani ambao wapo Timu ya Taifa wakimbadilishia Kocha Aussems Progaram yake ya mazoezi.
Simba walikuwa kwenye mapumziko ya siku mbili ambapo jana Septemba 16 wameanza mazoezi katika kiwanja cha Gymkhana wakiwa na baadhi ya wachezaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment