October 10, 2019


Mwamuzi wa kati aliyechezesha mchezo wa lgi kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union, Abubakari Mturo, amekuwa mmoja ya wale watalioorodheshwa majina yao kwenda katika Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa ajili ya mafunzo ili kupata beji.

Mturo aliongoza mchezo huo ambao ulileta gumzo juu ya bao alilofunga Abdulaziz Makame ambalo wengi walikuja juu na kudai kuwa halikuwa bao halali.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi nchini, Salum Chama, amesema kuwa Mturo ni moja ya waamuzi ambao watakuwa kwenye mafunzo hayo.

"Mpango wetu hivi sasa ni kuona waamuzi wanapata semina nyingi zitakazowafanya wawe na uelewa mkubwa.

"Tayari tumepeleka majina FIFA kwa ajili ya kupewa semina pamoja na wale ambao watapewa beji ni pamoja na waliochezesha mechi ya yanga dhidi ya Coastal Union.

1 COMMENTS:

  1. haya ninyi mliokuwa mnakomaa goli lifutwe mmepata majibu, mwamuzi huyo anakwnda kupewa beji ya fifa. utashangaa walalamikaji sio coastal union ni hawa lopolopo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic