MBONA WATANYOOKA!! MAJEMBE YANGA YAREJEA
Hatimaye wachezaji wa Yanga, Issa Bigirimana, Rafael Daud na Paul Godfrey wamerejea mazoezini kunako kikosi cha Yanga.
Ikumbukwe watatu hao waliumia nyakati tofauti wakiwa katika harakati za kuitumikia timu yao kwenye mechi za ligi.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema kuwa wachezaji hao wamerejea na tayari wameshaanza mazoezi mapesi kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za ligi na mashindano mengine.
"Wachezaji wetu walioumia wako fiti na tayari wamesharejea mazoezini.
"Daudi, Bigirimana na Boxer wote wamejiunga na kikosi na tayari wameshaanza mazoezi mepesi kwa ajili ya mechi zijazo."
Kurejea kwa wachezaji hao inakuwa kama ni neema kwa Yanga kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri.
Yanga itakutana na timu hiyo mechi ya kwanza ikichezwa Oktoba 27 kabla ya kurudiana nao waarabu hao Novemba 03.
0 COMMENTS:
Post a Comment