UONGOZI wa
Azam FC umesema kuwa hauna presha na michezo yao ya ligi kwa kuwa wamejipanga
kufanya vema jambo linalowapa nafasi ya kujiamini kupata matokeo chanya kwenye
michezo yao yote.
Mpaka sasa
Azam FC imecheza jumla ya michezo mitatu sawa na dakika 270 kwenye ligi na
imeshinda yote imejikusanyia pointi tisa kibindoni huku ikiifukuzia rekodi ya
Simba ya bila kupoteza kimyakimya.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’
amesema kuwa wanatambua ligi ina ushindani mkubwa nao wanapambana kwa kasi
kupata matokeo chanya.
“Tumerejea
rasmi kwenye ligi na tulianza kazi yetu mbele ya Ndanda tukamaliza na Namungo
kazi inayofuata ni mbele ya JKT Tanzania hesabu zetu ni kufanya vizuri.
“Tunaamini
katika kile ambacho tunakifanya, wachezaji na benchi la ufundi linafanya kazi
kwa ushirikiano hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kazi bado
inaendelea,” amesema Popat.
Azam FC
kwenye michezo mitatu imefunga mabao matano na imefungwa bao 1 ikiwa na pointi
tisa kibindoni kwa sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment