JACKSON Mayanja, aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba na
Coastal Union kwa sasa yupo ndani ya KMC amesema kuwa wachezaji wa Yangawanapaswa
kujipanga kufuta makosa yao kimataifa kwa kufanya vema kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na
Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Yanga
imeondolewa kwenye mpango wa Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa na Zesco sasa
ipo ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika na makundi yanatarajiwa kufanyika
nchini Misri Octoba 10.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa wawakilishi wa Tanzania wana kazi
ngumu ya kufanya kwenye michuano ya kimataifa kutokana na ushindani uliopo
kwenye michuano ya kimataifa.
“Michuano ya
kimataifa ni tofauti na ligi yetu ambayo tunaicheza kwa sasa hivyo timu
itakayopata fursa ya kupeperusha bendera ni lazima ijipange kisawasawa kwani
matokeo yanabebwa na maandalizi.
“Natambua
kwamba kila timu inahitaji matokeo ndio maana inashiriki ila ugumu kwenye
michuano ya kimataifa ukishindwa kutumia vema uwanja wa nyumbani kuna ugumu
kwenye michezo ya nje,” amesema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment