BAADA YA KUONDOLEWA CAF, ZAHERA AJA NA MALENGO MENGINE KUREJESHA FURAHA
Mjipange! Ndiyo kauli aliyoanza nayo Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa kwa sasa anaelekeza nguvu zake kusaka pointi kwenye Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kukiondoa kikosi hicho kwenye nafasi ya mwisho ambayo wanashikilia.
Kocha huyo ameweka wazi jambo hilo ikiwa ni baada ya kumaliza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zesco United, juzi Jumamosi nchini Zambia.
Yanga kwenye ligi imecheza mechi moja pekee ambayo ilipoteza mbele ya Ruvu Shooting na sasa wapo nafasi ya mwisho kati ya timu 20 ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haina pointi.
Zahera amesema kuwa akili yake kwa sasa anajikita kwenye ligi ambapo wanakuja kwa ajili ya kusaka ushindi katika michezo yao.
“Kwa sasa tunarudi kujiandaa na ligi na lengo letu ni kushinda kwa sababu tuko chini katika msimamo.
0 COMMENTS:
Post a Comment