October 1, 2019


Ni kama msala kwa Yanga ambayo imetoka kutolewa kunako Ligi ya Mabingwa Afrika Jumaosi iliyopita kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Zesco United ya Zambia.

Msala huo umetokea mara baada ya beki wake Mghana, Lamine Moro kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumchezea rafu mshambuliaji wa Zesco.

Kuonyeshwa kwa kadi nyekundu hiyo kwa Moro, kunamfanya sasa akose mechi mbili za Kombe la Shirikisho Afrika ambalo Yanga wameangukia hivi sasa.

Mmoja wa waamuzi wanaotambulika na FIFA hapa nchini, alisema Moro atazikosa mechi hizo ambazo zitakuwa ni za shirikisho za kuwania hatua ya makundi.

Droo ya makundi ambayo inasubiriwa kwa hamu na wadau wa soka hapa Tanzania, inatarajiwa kupangwa Oktoba 9 mwaka huu.

7 COMMENTS:

  1. Waandishi nyie ni wazushi kichwa cha habari kinachonganisha eti CAF yaiumiza Yanga....kwanini msingesema tu Lamine atakosa mechi za mtoano kuingia makundi

    ReplyDelete
  2. Harafu hajapewa straight red card anakadi 2 za njano anakosa game 1 kamaaa ingekua kadi ya moja kwa moja ni mech 3 acheni kutudanganya

    ReplyDelete
  3. Kwann uandike usichokua na uhakika? Kaaazi kwelikweli...

    ReplyDelete
  4. Hahahahah! This is Saleh Jembe Blog!!!

    ReplyDelete
  5. sasa kama hana shule ya kutosha kwa nn asitoe pumba zilizoko kichwan mwake?
    kila siku tumalaumu mambo haya

    ReplyDelete
  6. Ni mechi moja tu hii siyo kadi yamoja kwa moja alipewa njano mbili tuebooh

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic