October 1, 2019


Utata kwisha! Baada ya kuwepo kwa sintofahamu juu ya uraia wao, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani Idara ya Uhamiaji (Migration), imetoa tamko juu ya uraia wa watoto wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ na Prince Nillan aliozaa na mjasiriamali wa nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Hivi karibuni yaliibuka maswali mengi kutoka kwa wadau mbalimbali baada ya Zari kutangaza kuwa watoto wake wote ni raia wa Afrika Kusini ‘Sauz’ anakoishi nao.

Baada ya kuibuka kwa maswali hayo na kukosa majibu yasiyo rasmi hasa kwa mtoto wao wa kwanza, Tiffah Dangote ambaye alizaliwa Bongo, lakini mama yake amekuwa akikisisitiza kuwa ni raia wa Afrika Kusini, Gazeti la Ijumaa Wikienda liliamua kumaliza utata huo kwa kuitafuta mamlaka husika ambayo ilitoa ufafanuzi.

Akizungumza na wanahabari wetu kuhusiana na uraia wa watoto hao wa Diamond, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Mratibu Mwandamizi, Ally Mtanda alikuwa na haya ya kusema;

“Huyo Zari kama anasema watoto hao wote ni raia wa Afrika Kusini, hakosei, yuko sahihi kwa kuwa yeye anaishi nchini humo, hivyo watoto wake wana uraia wa kurithi kutoka kwake.

“Lakini hata hivyo, kwa kuwa watoto hao baba yao ni Mtanzania, pia wana uraia wa Tanzania ambao wameurithi kutoka kwa baba yao hivyo wana uraia wa nchi mbili na wanaruhusiwa kuwa na pasipoti ya Tanzania na Afrika Kusini kwa wakati mmoja.

“Watoto watatakiwa kuukana uraia wa nchi moja na kubaki na uraia wa nchi moja baada ya kutimiza umri wa miaka 18 ambapo watakuwa na uamuzi wa kuchagua uraia wa baba au mama yao.”

Msemaji huyo aliwataka Wabongo kutoshtushwa na kauli za Zari kwamba watoto wake hao ni raia wa Afrika Kusini hivyo ukweli ni kuwa wana uraia wa Tanzania pia.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic