October 1, 2019


Mfungwa mmoja amefariki na wengine saba kujeruhiwa baada ya gari la magereza kupinduka huko Kathageri karibu na Daraja la Thuci, Wilaya ya Embu, leo.

Pia askari watano wa magereza walipata majeraha na kupelekwa pamoja na wafungwa waliojeruhiwa, katika Hospitali ya Rufaa ya Chuka.

Ofisa mfawidhi wa Gereza la Embu, Henry Ochieng, alisema lori hilo lilipinduka mara mbili wakati likiwa kwenye mteremko.

Aliongeza kwamba wafungwa hao walikuwa wakisafirishwa kutoka Gereza la Embu kwenda Mahakama za Meru ambapo pia dereva alijeruhiwa vibaya na kupelekwa kwa matibabu katika Embu Level Five Teaching and Referral Hospital.

Shuhuda, Maureen Mwende, alisema ajali hiyo ilitokea asubuhi wakati wa mvua.

“Nafikiri ni kutokana na utelezi gari likashindikana kudhibitiwa,” alisema mwanamke huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic