ZAHERA APEWA AHUENI NA MOLINGA
Moto alioanza nao mshambuliaji wa Yanga, David Molinga 'Falaco' katika mechi ya ligi dhidi ya Polisi Tanzania jana imeanza kumpunguzia deni Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera la kutokatwa mkono wake.
Molinga jana aliibuka shujaa akiisaidia Yanga kusawazisha baada ya kufunga mabao mawili na kuufanya mchezo uwe na matokeo ya 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania.
Sare hiyo imeanza kumpa ahueni Zahera aliyeahidi kuwa endapo Falcao asipofunga mabao matatu msimu huu akatwe mkono wake mmoja.
Zahera alitoa ahadi hiyo kabla ya msimu wa ligi kuanza akiamini Falcao ni mkali ndani ya dimba dhidi ya Heritier Makambo ambaye alikuwa anaichezea.
Kwa kufunga mabao mawili jana, Molinga sasa amebakiza mabao 13 pekee kufikisha 15 ambayo Zahera aliahidi Molinga kufunga.
Nakumbuka Zahera aliahidi mabao 25 na sio 15 ili kunusuru mkono wake
ReplyDeleteHahahahaaaaa Zahera bwana ajiangalie mkono usije ukakatwa
ReplyDelete