October 9, 2019


Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameibuka na kukosoa baadhi ya wachezaji wake ndani ya timu hiyo.

Zahera ameeleza kutofurahishwa na viwango vya wachezaji hao kutokana na mwenendo wa matokeo ambayo wameyapata katika mechi za ligi.

Mpaka sasa Yanga imecheza jumla ya mechi tatu na ikiw aimejikusanyia alama 4 pekee.

Kutokana na matokeo hayo, taarifa imesema Zahera ameanza kuwalalamikia baadgi ya wachezaji hao kuwa wamekuwa wakifanya uzembe unaoipeleka pabaya Yanga.

Aidha, imeelezwa pia Zahera amesema ili timu iweze kufanikiwa ikiwemo kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu inawapasa wachezaji wapambane na wajitume kwa faida ya yanga ili ifikie malengo yake.

5 COMMENTS:

  1. Kuwachana wachezaji ni sawa, ila na wao wakuchane mfumo wako haufai.

    ReplyDelete
  2. Kocha ana matatizo ya mfumo na kuchezesha wachezaji out of position. Kingine anachukua muda mrefu sana kufanya sub hata kama timu imeelemewa. Kwa mfano game na Coastal ilikuwaje Kaseke akaendelea kucheza wakati alionekana kachoka?

    Kaseke kaumia bado tu wakamrejesha uwanjani kama vile hakukuwa na wachezaji wengine wenye uwezo zaidi yake?

    ReplyDelete
  3. Kitu ambacho wanakosea sana ni kumchezesha Yondani kila game, yule umri umeenda inatakiwa awe anapumzishwa baadhi ya mechi ili kumpa nguvu ya kucheza vizuri zile game muhimu.

    ReplyDelete
  4. Huyu mwandishi anawazingua tu. Zahera Hajamchana mchezaji yeyote.
    si somi tena hizi habari Fuck you Salehe

    ReplyDelete
  5. Tunamshauri Zahera kusimamia mazoezi kikamilifu na kuwa na mbinu ya ukocha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic