December 23, 2019


MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Azam FC leo watakuwa na kazi ya kutetea ubingwa wao kwa kucheza mchezo wa kwanza wa hatua ya 62 bora dhidi ya African Lyon utakaopigwa uwanja wa Uhuru.
Azam FC ilitwaa ubingwa huo kwa kuichapa bao 1-0 Lipuli lililopachikwa kimiani na Obrey Chirwa ambaye yupo kwenye kikosi hicho akiwa ametupia mabao matatu tu ndani ya Ligi Kuu Bara na kutoa pasi moja ya bao.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ushindani na wanatambua kwamba ni mabingwa watetezi lazima watetee taji.
“Tunaheshimu wapinzani wetu na tunajua ni timu nzuri ndio maana inashiriki hii michuano na uzuri ni kwamba hapa kila mmoja anacheza fainali kwani atakayepigwa anatolewa jumla nasi lazima tupambane.
“Wachezaji wapo vizuri na kila mmoja anatambua kazi aliyopewa na mwalimu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao itakapoanza safari ya kuutetea ubingwa,” amesema Amin.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic