RASHID Juma, mshambuliaji wa Simba yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na uongozi wa timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC wakati huu wa dirisha dogo la usajili.
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kwa sasa Juma amekuwa hana namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho hivyo ataelekea KMC kujiongezea uzoefu.
“Juma mambo yake ndani ya Simba msimu huu haujawa sawa na tumefanya mazungumzo na baadhi ya timu ambazo zinahitaji huduma yake kwa sasa ikiwa ni pamoja na KMC ambao wameonyesha nia ya kumtaka,” alisema.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Juma alisema kuwa kwa sasa ameskia juu ya yeye kuhitajika na KMC ambao wameonyesha nia ya kuipata saini yake.
“Nimeskia juu ya habari za KMC kuitaka saini yangu, tuliwahi kuzungumza nao mwanzo ila kwa sasa sijazungumza nao hivyo ni jambo la kusubiri kuona nini kitatokea kwani kazi yangu mimi ni mpira, kama wananitaka kwa sasa watazungumza na viongozi wangu wa Simba” alisema Juma.
0 COMMENTS:
Post a Comment