December 3, 2019


Taarifa zilizopo hivi sasa ni kuhusiana na Kocha Msaidizi wa Simba, Denis Kitambi kuwa anaweza kuondolewa ndani ya kikosi cha kwanza.

Habari za ndani zinasema Kitambi ataondolewa ili kupelekwa katika kikosi cha vijana, Simba B na nafasi yake inaelezwa Suleiman Matola anaweza kuchukua nafasi yake.

Kitambi alichukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo, Masoud Djuma kutoka Burundi kushindwa kuelewana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa wakati huo, Pierre Lechantre.

Simba hivi sasa ipo katika mchakato wa kusaka Kocha Mkuu ambaye atachukua nafasi ya Patrick Aussems ambaye ameondolewa ndani ya klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic