December 29, 2019



UONGOZI wa Coastal Union umesema kuwa upo sokoni kutafuta majembe matatu ya kazi ili kuongeza ukali wa kikosi hicho chenye ngome yake mkoani Tanga.

Coastal Union ipo nafasi ya sita baada ya kucheza mechi 13 imejikusanyia jumla ya pointi 20 itacheza kesho na Mbeya City uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Akizungumza na SpotiXtra, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda alisema kuwa hesabu kubwa kwa timu ni kuongeza nguvu kwa kusajili wachezaji watatu ambao wataongeza kasi ya ushindani.

“Kila timu inafanya usajili kulingana na mahitaji yake, kwa namna kikosi chetu kilivyo hakihitaji maboresho makubwa kwani wachezaji wake wengi wameanza kuzoeana na kufanya kazi kwa ukaribu nitaongeza wachezaji watatu pekee.

“Nafasi zote zina wachezaji ambao nawaamini ila nikipata mshambuliaji mmoja, kiungo mshambuliaji na mkabaji hapo kikosi kitakuwa kwenye ubora wake, ila ikishindikana nitapandisha vijana wangu wa timu ya vijana,” alisema Mgunda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic