December 27, 2019



MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa ana imani na wachezaji wake wote licha ya kuanza kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Bournermounth kwenye mechi ya Ligi Kuu England.

Dany Gosling alianza kufunga bao la kwanza kwa Bournermouth dakika ya 35 lililowapeleka Arsenal vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma kwa bao hilo.

Nahodha wa Arsenal, Pierre Aubameyang alisawazisha bao hilo kipindi cha pili dakika ya 63 na kuwafanya wagawane pointi moja wakiwa ugenini.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Arteta kukaa benchi akiwa na Arsenal baada ya kupewa kandarasi ya miaka mitatu na nusu.

"Wamefanya vema vijana wangu na wameanza vizuri katika mchezo wetu wa ushindani, nina amini watafanya mambo makubwa hapo baadaye ni suala la muda tu," amesema. 

Arsenal ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 19 wapinzani wao Bournernouth wapo nafasi ya 16 wana pointi 20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic