December 27, 2019



JURGEN Klopp,Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kushinda mbele ya wapinzani wao Leicester City kwenye uwanja wao wa King Power.

Liverpool imezidi kujikita kileleni baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi Leicester City.

Mabao ya Liverpool yalipachikwa kimiani na Roberto Firmino aliyepachika mabao mawili dakika ya 31 na 74, James Milner kwa mkwaju wa penalti dakika ya 71 na Trent Alexander-Arnold dakika ya 74 alipachika msumari wa mwisho kwa Liverpool.

"Sio kazi rahisi kupata matokeo kwa timu bora ambayo ipo vizuri, kikubwa ni kwamba tulitakiwa kushinda kwa kuwa tunahitaji kufikia hatua nyingine ya ushindani ni jambo la furaha kwetu kushinda," amesema.

Ushindi huo unaifanya Liverpool iliyocheza mechi 18 kufikisha jumla ya pointi 52  huku Leicester City ikibaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 39 imecheza mechi 19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic