December 29, 2019



UONGOZI wa KMC umesema kuwa unapata tabu kupata pointi tatu kwenye mechi zake za sasa kutokana na ugumu wa ratiba pamoja na ushindani uliopo kwa sasa ndani ya ligi.

KMC iliyopanda daraja msimu wa 2018-19 imekuwa na mwendo wa kusuasua msimu huu kwani ilipokea kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Polisi Tanzania na jana ilipoteza mbele ya Simba uwanja wa Uhuru kwa kufungwa mabao 2-0.

Kaimu Kocha Mkuu, Ahmad Ally amesema wanaumia na matokeo ambayo wanayapata ila hawana namna ya kufanya kutokana na ligi kuwa ngumu na ratiba kutokuwa rafiki kwao.

“Tumesafiri kutoka Moshi tukaja kucheza na Simba Dar ni mechi ngumu na kila mchezaji anatambua kwamba tunahitaji ushindi ila matokeo kwetu sio rafiki, nina imani haya yote yatakwisha tutarejea kwenye ubora," amesema.

KMC ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 9 baada ya kucheza mechi 13 za Ligi Kuu Bara msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic