UONGOZI wa
Ndanda FC umesema kuwa utatibua rekodi
mabingwa watetezi Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 31 baada ya
kucheza mechi 12 ikiwa chini ya Sven Vanderbroek ambaye ameongoza mechi tatu
bila kufungwa akiwa kwenye benchi.
Sven raia wa Ubelgiji alichukua
mikoba ya Patrick Aussems aliyetimuliwa ndani ya Simba ameanza kwa kasi ambapo
kwenye jumla ya mechi tatu za mwanzo sawa na dakika 270 hajafungwa zaidi ya
kujikusanyia mabao 12 atamenyana na Ndanda leo, Desemba,31 uwanja wa Taifa.
Simba ikiwa
chini ya Sven alianza kuiongoza kwenye mechi dhidi ya Arusha FC iliyokuwa ya
Kombe la Shirikisho na ilishinda mabao 6-0, kwenye mechi mbili za ligi kuu
mbele ya Lipuli ilishinda mabao 4-0 pia ilishinda mabao 2-0 mbele ya
KMC mechi zote zilichezwa uwanja wa Uhuru.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ndanda FC iliyo nafasi ya 19 na pointi
nane, Idrisa Bandari amesema kuwa kikosi kipo imara hakitishwi na rekodi
zinazowekwa na mtu yoyote zaidi ya kupigia hesabu pointi tatu.
“Maandalizi
yetu sisi siku zote ni kuona kwamba timu inapata matokeo chanya na kushinda
bila kuangalia rekodi ambazo zinawekwa, hakuna kinachotuogopesha kwa wapinzani
wetu tutapambana kupata pointi tatu muhimu mbele ya Simba,” amesema Idrisa.
Tuliahidi kutibuwa kama wanavoahidi wa Jangwanic lakini tukatibuliwa na wa jadi wanaombwa kuroweka nywele kwa sabuni ili uwembe usiikekete kichwa
ReplyDelete