December 28, 2019


STANSLAUS Mabula, mbunge wa Nyamagana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi leo kwenye mashindano ya Riadha ya Taifa ya Ngorogoro Crater National Athletics Championship.

Mashindano hayo yanataraajiwa kuanza kutimua vumbi leo mkoani Mwanza yatashirikisha mikoa zaidi ya 13 katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Tullo Chambo amesema kuwa mwamko umekuwa mkubwa kutokana na mikoa mingi kujitokeza kusaka vipaji vipya,

"Mikoa ya Morogoro, Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Ungunja, Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Mwanza, Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo imeshawasili na mingine tunatarajia kupokea leo, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic