December 28, 2019


UONGOZI wa Simba umesema kuwa umejipanga kupata pointi tatu lo mbele ya KMC mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru.

Jana,Simba imefanya mazoezi ya mwisho uwanja wa Simba Mo Arena.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao wote ila kikubwa ni pointi tatu.

"Tunawaheshimu wapinzani wetu wote ila hamna namna tunahitaji pointi tatu mashabiki watupe sapoti," amesema. 

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 28 imecheza jumla ya mechi 11 itamenyana na KMC iliyo nafasi ya 17 na ina pointi tisa kibindoni baada ya kucheza mechi 12.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic