Miamba ya soka nchini, Simba na Yanga imetenganishwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyopangwa wiki jana huku ikiangukia kuvaana na Mtibwa Sugar na Azam FC.
Katika ratiba hiyo, waandaaji wa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 5 hadi 13, mwakani, Yanga imepangwa Kundi A pamoja na mabingwa watetezi Azam FC, Jamhuri ya Pemba na Mlandege ya Unguja.
Wanafainali wa msimu uliopita, Simba wapo Kundi B pamoja na Mtibwa Sugar, Zimamoto na Chipukizi za Zanzibar.
Katika taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar, Omar Hassan Omar ‘King’, pia imetangaza kamati ya kusimamia mshindano hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi ametajwa kuwa ni Sharifa Khamis Salim na Katibu wa Kamati hiyo ni Khamis Abdulla Said.
Wajumbe wa Kamati ya michuano hiyo itakayofanyika visiwani Zanzibar, ni Khamis Mussa Omar, Issa Mlingoti, Seif Kombo Pandu, Mohamed Ali Hilali (Tedy), Aiman Othman Duwe, Fatma Hamad Rajab, Salum Ubwa Ali Khalil, Juma Mmanga na Suleiman Pandu Kweleza.
Aliye elewa tafadhali
ReplyDeleteHakuna kitu hapo hizo kozi za miezi 3 ndio umeshakuwa mwandishi
ReplyDelete