Juzi mida ya jioni hivi, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mnyarwanda, Patrick Sibomana alikuwa akiperuzi kwenye Instagram ghafla akakutana na picha za fundi Haruna Niyonzima akiwa na uzi wa Yanga, hapohapo jamaa akatikisa kichwa na kusema wamekwisha.
Yanga ilifanikisha usajili wa Niyonzima juzi Alhamisi usiku baada ya kufikia muafaka mzuri akitokea AS Kigali ya Rwanda iliyokubali kumuachia baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita.
Kutua kwa Niyonzima kutaimarisha safu hiyo ya kiungo iliyokuwa inachezwa na Issa Mohamed ‘Banka’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Raphael Daudi na Papy Tshishimbi.
Sibomana alisema ana matarajio makubwa ya kuiona Yanga ikicheza soka safi la pasi na kushambulia huku wakipata matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.
Sibomana alisema muda mrefu alikuwa na ndoto za kucheza timu moja na Niyonzima, hivyo anaamini ndozo zake zimefanikiwa kwa kukutana Yanga ambayo ni moja ya klabu kubwa Afrika.
“Kila mtu anafahamu kuwa Niyonzima ni mchezaji wa namna gani, imekuwa jambo nzuri kwangu kumuona katika klabu hii, nilikuwa natamani siku moja nipate nafasi ya kucheza naye katika timu moja, bahati nzuri nafasi hiyo nimeipata na sina budi kuitumia vizuri.
“Kilichobakia hivi kuitumikia timu yetu ya Yanga kwa pamoja na ushirikiano mkubwa ili tufikie malengo yetu, kwani Niyonziama ni kama kaka yangu mengi nimekuwa nikijifunza kupitia kwake.
“Hivyo kama usajili wake umefanikiwa, basi tarajia kuiona Yanga mpya itakayopambana kupata matokeo mazuri ya ushindi baada ya usajili wake kukamilika na kutambulisha,” alisema Sibomana ambaye hucheza timu ya Taifa ya Rwanda na Niyonzima.
0 COMMENTS:
Post a Comment