Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa kauli ambayo ni kama ‘Marry Christmas’ ya mapema kwa Wanayanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya TFF, Elias Mwanjala ameliambia Spoti Xtra kuwa wachezaji wote waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa hivi karibuni wataruhusiwa kucheza ili mradi tu usajili wao uwe umekamilika.
Mwanjala alisema kuwa hakuna mchezaji atakayezuiwa kutumikia timu yake mpya endapo usajili wake utakuwa umekamilika kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa tafsiri ambayo huenda ikawapa faida Yanga kuelekea mechi ya Simba, Januari 4.
“Hatutaki kuona mchezaji anashindwa kuitumikia timu yake kwa sababu tu amechelewa kupata kibali.
“Tutakachoangalia ni usajili wa mchezaji husika ukamilike kwa kila kitu, baada ya hapo ataruhusiwa, tumejipanga kwa hilo na ni matumaini yetu kuwa hakuna kitakachoharibika, jambo la msingi ni timu kufuata taratibu,” alisema Mwanjala na kuongeza kuwa:
“Huko nyuma kulikuwa na ulazima kusubiri kamati ipitie sajili zote ila kwa sasa hakutakuwa na mlolongo kama huo tena, tumeamua kufanya hivyo kwa sababu ligi haitasimama wakati huo wa usajili,” alisema na kuongeza kama kuna klabu inadaiwa na mchezaji haitaruhusiwa kutumia usajili mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment