December 29, 2019


Imeelezwa kuwa Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amethibitisha kuwa ameishtaki klabu hiyo katika Shirikisho la soka duniani (FIFA).

Taarifa imeeleza, kwa mujibu wa kanuni alivyofuatilia, Zahera ana uhakika kuwa watamlipa mara mbili ya pesa anazodai kutokana na usumbufu aliopata.

Wakati akiwa Kocha wa Yanga, Zahera alihusika katika kusaidia kulipa baadhi ya fedha ndani ya timu hiyo ikiwemo za safari na chakula wakati wakiwa kambini.

Ikumbukwe hivi karibuni alikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufuatilia madai yake lakini hakupata ushirikiano wowote kutoka kwa mabosi wake wa zamani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic