ADEYUM
Suleiman, beki wa kushoto wa Yanga alitumia dakika 45 tu kuiondoa jumla timu ya
Jamhuri, kwenye mbio za kuwania Kombe la Mapinduzi linalofanyika Visiwani
Zanzibar, baada ya kufunga bao la kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-0 waliyopata Yanga.
Bao la
kwanza alilifunga Adeyum kwa mpira wa adhabu akiwa nje ya 18 kwa kupiga shuti
kali lililozama moja kwa moja langoni huku likimuacha mlinda mlango wa Jamhuri
akilisindikiza kwa macho dakika ya 45.
Kuingia kwa
Mohamed Issa ‘Mo Banka’ dakika ya 79 akichukua nafasi ya Mapinduzi Balama
kuliongeza kasi ya mashambulizi ambapo kiungo huyo alitumia dakika sita
kuifungia timu yake bao lake la pili .
Mchezo huo
uliochezwa Uwanja wa Amaan, ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kupambana
kutafuta matokeo ila bahati haikuwa kwa Jamhuri kwani uimara wa mlinda mlango
wa Yanga, Ramadhani Kabwili uliwazuia kupata mabao.
Yanga sasa
inatinga hatua ya nusu fainali inayotarajiwa kuchezwa Ijumaa, Januari 10,
Uwanja wa Amaan dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo ilishinda mbele ya Chipukizi
kwenye mchezo wa robo fainali baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya
dakika 90 na Mtibwa Sugar ilishinda kwa penalti 4-1.
Kwa ushindi
wa Yanga unafanya timu zote za Visiwani Zanzibar msimu huu kuishia kwenye hatua
ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya Mlandege kutolewa na mabingwa
watetezi Azam FC itakayomenyana na
Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment