SIMON Msuva amepata dili la kujiunga na klabu ya Benfica inayoshiriki Ligi Kuu ya Ureno kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Kwenye dili hilo nyota huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania aliyekuwa anakipiga Yanga pia kabla ya kutimkia Difaa El Jadidi ya Morocco hatawapa hata mia mbovu mabosi wake wa zamani Yanga.
Yanga wakati wa kumuuza Msuva 2017 kwenda Difaa El Jadida walishauriwa na meneja wa Msuva wamuuze dola 80,000 (Tsh 180M) ili waweke kipengele cha kupata mgao akiuzwa kwingine (Benfica) ila walikataa na kulipwa dola 100,000 (Tsh 229M).
Simba ilipata mgawo kutoka TP Mazembe wakati Samatta aliposajiliwa na KRC Genk ya Ubelgiji mwaka 2016 na kusababisha African Lyon waamke na kusema ni mchezaji wao na si wa Simba.
Dr. Jonas Tiboroha amesema kuwa ni kweli Msuva amejiunga na Benfica kwa mkataba wa miaka mitatu ataapelekwa Panathnaikos ya Ugiriki kwa mkopo.
0 COMMENTS:
Post a Comment