January 8, 2020

SADIO Mane, mchezaji Bora wa mwaka 2019 kwa Afrika amesema kuwa shukrani zake zote anazirudisha kwa Kocha Mkuu wa Senegal, Aliou Cisse na wachezaji wenzake wa Liverpool pamoja na mashabiki zake wote duniani bila kuwasahau watu wake wa Senegal.

Mane amesema "Mpira ni kazi yangu, naipenda na nina furaha ya kweli katika hili, shukrani kwa kocha wa timu yangu ya Senegal, wachezaji wenzangu, watu wa Senegel kwa kunipa msukumo katika kazi yangu," amesema.

Mane ametwatwaa tuzo hiyo ilyokuwa ikishikiliwa na Mohamed Salah, mchezaji mwenzake wa Liverpool raia wa Misri ambaye alitwaa tuzo hiyo mara tatu na ni mchezaji pekee Afrika aliyechukua tuzo hiyo mara nyingi ila hakutokea kwenye usiku wa tuzo.

Tuzo zilikwenda kwa hawa hapa namna hii:-. 
Mchezaji Bora wa mwaka 2019 Afrika kwa upande wa Wanaume:- Sadio Mane.
Mchezaji Bora wa Mwaka 2019 Afrika kwa upande wa Wanawake:- Asisat Oshoala
Mchezaji mdogo wa Mwaka 2019: Achraf Hakimi
Timu ya Mwaka 2019: Onana, Aurier, Matip, Koulibaly, Hakimi, Gueye, Mahrez, Zyech, Salah, Aubameyang, Mane.
Bao bora la Mwaka: Mahrez (Pigo huru kwenye michuano ya Afcon)
Kocha wa Mwaka: Djamel Belmadi
Kocha Bora wa Mwaka kwa upande wa Wanawake: Diseree Ellis.

2 COMMENTS:

  1. Salaa mbinafsi na anachoyo,kwa nini hakutokea kwenye tuzo,anaroho mbaya sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alikuwa IRAN kwenye mazishi ya Jenerali Qasem Soleiman

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic