January 16, 2020


SAID Khamis Jr mshambuliaji wa Mbao FC leo ana kazi kubwa ya kuendeleza ubabe wake aliouanza msimu wa mwaka 2018/19 uwanja wa CCM Kirumba kwa kumtungua mlinda mlango, Aish Manula bao 1-0 na kuipa pointi tatu timu yake.
Leo, Sven Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ana kibarua kizito cha kukutana na fupa hilo la Mbao ambalo lilimshinda Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji.
Akizungumza na Salh Jembe, Jr amesema kuwa maandalizi yapo vizuri kwa timu yake ni suala la muda tu kuona namna gani watapata pointi tatu mbele ya Simba.
“Tumejipanga na tupo tayari kupata matokeo, msimu huu tumekuwa na mwenendo mgumu hii inatokana na ushindani wa ligi ila tupo tayari na tutapambana kufanya vizuri,” amesema Jr.

Simba inakutana na Mbao leo Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa msimu uliopita kwa bao 1-0 jambo lililowakasirisha mashabiki na kumtupia makopo Aussems ambaye kwa sasa yupo zake nchini Ubelgiji.

3 COMMENTS:

  1. Hata uchochee kaa ukijua kamwe mpira hauna mwenyewe,kwani huyo mbao ameshafungwa mara ngapi na simba tena magoli mengi mbona hujachukua kumbukumbu za simba kumfunga mbao ukaanadika?acha ushabiki brother mbona simba inawatoa povu sana yani kuanzia magazet yenu mpaka huku kwenye social meia pia,amakweli yanga ni timu ya wananchi.

    ReplyDelete
  2. Bao la penalti ndio imekuwa kumtungua?Ushabiki wako wa wazi unajua kinyaa. Badilisha blog iitwe jina la timu yako pendwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic