January 18, 2020


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji ametangaza kwamba ataikimbia Ligi Kuu ya Tanzania Bara mapema kama wapinzani wao anaokutana nao wataendelea na staili ya kujiangusha na kupoteza muda ambayo kwake hajawahi kupendezwa nayo.

Kocha huyo ambaye ana wiki moja tangu alipotua nchini kuja kuziba nafasi ya Mkongomani Mwinyi Zahera amesema hatajali muda gani ambao atakaa ndani ya kikosi hicho lakini kama wapinzani anaokutana nao hawatabadilika na kucheza soka zuri, ataondoka na kuacha kufundisha.

Eymael ameweka bayana hilo baada ya kikosi chake kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara, juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Mbelgiji huyo ameliambia Championi Ijumaa kuwa ataacha kufundisha soka Tanzania na ataondoka mara moja kutokana na kutofurahiswa na aina hiyo ya uchezaji wa wapinzani wake ambapo anataka wacheze soka la kuvutia.

“Kama timu ambazo nitacheza nazo wataendelea kuanguka na kujilaza kwa ajili ya kupoteza muda nitaondoka na nitaacha kufundisha hapa Tanzania kwani ninapenda soka la kuburudisha.

“Wale tuliocheza nao (Kagera Sugar) kipa wao alikuwa anajiangusha bila hata sababu ya msingi, lakini hata wachezaji wao mimi sifurahishwi na hilo. Hata kama tunafungwa basi timu itawale na icheze soka zuri kama ambavyo sisi tunafanya na siyo vinginevyo,” alisema Eymael.


8 COMMENTS:

  1. Hakuna kocha hapo.

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa yupo vipi na lab da angelistahili kuyasema hayo Ingekuwa wachezaji wake ndio wenye tabia za kujiangusha lakini eti timu pinzani na hata Ingekuwa wachezaji wake ilibidi awakataze tu. Kwahivo wachezaji wa timu pinzani watazidi kujiangusha ili waone Yanga inasambaratika. Huyo kaelemewa na matukio na sasa anatafuta mbinu za kuingia mitini na kuiwacha timu isijuwella kufanya. Keeli ndugu hamna kocha hapo

    ReplyDelete
  3. Kipigo cha goli tatu kimempa kiwewe. Poleni watani ndio dunia ilivo lakini siku njema huonekana toka asubuhi. Kocha huyo Ana sifa ya kuhama Kutoka timu na kuhamia nyengine kwa kasi kubwa

    ReplyDelete
  4. sasa wewe kocha gani ambaye hujui kwamba ili timu pinzani wasijiangushe unatakiwa uwafunge. so walikuwa wanajiangusha wakiinuka wanakwenda kufunga mpaka zikafika tatu. Tuna bahati mbaya huyu ni Zahera mwingine.

    ReplyDelete
  5. Kiukwel huyu kocha bado atulie Kwanza akosome mchezo wa kibongo akicheza na Azam sindo atajinyonga kwa kipa wao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic