January 10, 2020


MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi kwa sasa inazidi kuchanja mbunga ambapo kwa sasa ipo hatua ya nusu fainali na leo kazi itakuwa kubwa ndani ya uwanja kutafuta timu itakayotinga hatua ya fainali.

Bingwa mtetezi wa kombe hili ni Azam FC ambaye naye ametinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mlandege bao pekee lililofungwa na Obrey Chirwa.


Vita kubwa itakuwa kwenye mechi itakayowakutanisha mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam FC mbele ya Simba iliyotinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Mlandege FC.


Jana, Uwanja Amaan, Mtibwa ilikata tiketi ya kushiriki fainali baada ya kushinda mbele ya Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza.


Mtibwa Sugar ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti 4-1 mbele ya Chipukizi baada ya dakika 90 kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, na ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penalti baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kwenye changamoto ya penalti Mtibwa Sugar ilishinda mabao 4-2 na kuifungashia virago jumla Yanga.

Haya hapa mambo yatakayofanya hatua ya nusu fainali ya pili  kati ya Simba na Azam FC kuwa ya kibabe kutokana na mambo haya hapa:-

Kisasi cha kukosa ubingwa
Simba mwaka 2019 iliaacha ubingwa ukibebwa na Azam FC baada ya kukubali kufungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali jambo lililofanya washindwe kufurukuta kwenye mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Mabao ya Azam FC yaliyoipa ubingwa Azam FC yalifungwa na Mudhathiri Yahaya aliyemalizia pasi ya Ennock Atta na bao la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa aliyemaliza pasi ya Nicolas Wadada.

Heshima ya kutwaa kombe
Mwaka 2020 hili linakuwa ni taji la kwanza kwa timu hizi zote kuanza kupigania jambo ambalo litafanya kila timu kupambana kufikia malengo ya kutwaa kombe la kwanza kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka 2020.

Kila Kocha hesabu zake ni kuona anafungua mwaka kipekee jambo ambalo litalowafanya wacheze kwa kujituma kufikia malengo kwa timu itakayotinga hatua ya fainali itajifungulia nafasi ya kutwaa kombe hilo.

Zawadi kwa mashabiki

Azam FC ilipomenyana na Simba kwenye mchezo wa ligi ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 jambo ambalo liliwakasirisha mashabiki wao.

Pia Simba walikuwa na matumaini makubwa ya kushinda mbele ya Yanga mchezo wao wa Januari, 4, 2020 mwisho wa siku waliambulia sare ya kufungana mabao 2-2 licha ya Simba kuanza kushinda.

Kitendo cha Yanga kuwafunga mabao mawili ndani  ya dakika saba ndicho kinachowauma mashabiki hivyo wachezaji watatumia nguvu nyingi kutafuta ushindi na kuwapa zawadi mashabiki.

Nafasi kwnye timu

Kwa sasa makocha wote wa Azam FC na Simba bado wanajenga vikosi vyao na kutafuta wachezaji wa kuunda kikosi cha kwanza.

Arstica Cioaba bado anakijenga kikosi chake ndio maana amekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kwenye kikosi chake.

Hata Sven Vanderbroeck wa Simba bado hajapata wachezaji wake anaowahitaji kikosi cha kwanza kutokana na kutokuwa na muda mrefu aliokaa nao. Michuano hii ya kombe la fainali itafanya wachezaji wote wapambane kuonyesha kitu walichonacho kwa makocha wao ili kuongeza nafasi ya kuwa ndani ya kikosi cha kwanza.

Tuzo za mchezaji binafsi

Kwa timu itakayotinga hata ya fainali na kutwaa kombe huwa kunakuwa na tuzo ya mchezaji bora na mfungaji bora. Mpaka sasa vita ya ufungaji haina mwenyewe kwani wafungaji wote wamefunga bao moja pekee.

Obrey Chirwa wa Azam FC, John Bocco, Ibrahim Ajibu na Sharaf Shiboub wa Simba, Mohamed Issa na Adeyum Suleiman wa Yanga, Haruna Chanongo wa Mtibwa Sugar na Suleiman Nassor wa Chipukizi wote wana bao mojamoja jambo linaloongeza vita kwa wachezaji wote isipokuwa Chipukizi wameshafungashiwa virago.

Fainali ya Kombe la Mapinduzi itakuwa Januari 13.

Kwenye michuano ya Mapinduzi ni timu za bara tu ambazo zitashiriki michuano hii baada ya Mlandege, Chipukizi, Zimamoto na Jamhuri na jana Yanga ilifungasha virago kufungashiwa virago kwenye hatua ya nusu fainali.


8 COMMENTS:

  1. Nianze kwakuwakosoa wajinga nyie mnaosimamia hii blog tena mkiongozwa na saleh,hivi inakuaje mnakosa umakini kiasi hiki kweli?mlandege amecheza na azam na akacheza na simba kweli?acheni kutudanganya jamani mnajipunguzia credibility,fans wengi wa hii blog wanaichukia sasaivi kwasababu ya mambo makuu mawili,1:ushabiki wa nje nje hapa namaanisha uyanga na usimba,nijuavyo mimi ukiwa mwandishi basi huna budi kuficha hisia zako pale unapokua kazin maana ukiweka ushabiki basi utajikuta umebaki wewe na mashabiki wenzako,2:umakini katika kazi zako brother,kadri siku zinavyokwenda inaonekana ndio unazid kupoteza ubora katika kazi yako,hii inaashiria wazi kwamba mengi yanayofanyika humu wewe kama mhariri hujui lolote maana kiti hiki kinaonekana kuna uliempa akalie,hatimae anafanya ujinga,na kama sio hivyo basi umesharidhika na kidogo ulichonacho maana inawezekana umeshajenga kanyumba ka 10milion mtoto anasoma st kunani na unakula broiler,unatembea kwa matako,vijana wengi sana wa kitanzania mnajisahau mapema sana yani mkishapata three basic needs it is over.but let me try to advice you my dude "IF YOU WANT TO SEE FAR YOU MUST STAND IN THE SHOULDER OF THE GIANT"ni ushauri tu inawezekana umeshakwama kifikra tafuta watu wenye mitazamo mikubwa wakusaidie,fanyia kazi brother utanikumbuka.

    ReplyDelete
  2. Narudi tena kwenye suala la mchezaji bora kama mmekua mkiangalia au kufuatilia mashindano haya ya mapinduzi cup mpaka sasa mchezaji bora anajulikana,vigezo vya mchezaji bora ni muda alioshiriki katika mechi na juhudi binafs alizoonyesha mchezaji huyo,mpaka sasa namuona IBRAHIM AJIBU akiwa ndio kinala wa haya,kwanini AJIB?kwanza amefunga goli kama mnakumbuka na pili amehusika kwenye magoli yote ya simba,AJIB ndie aliyetoa asist zote zilizosababisha magoli ya simba kwa mwenye kumbukumbu ataunga mkono hapo,ila bado tuangalie leo itakuaje,mdijaribu kuukwepa ukweli kwakujifanya eti hamumjui mchezaji bora mpaka sasa ikiwa mna kumbukumbu ya ajib.huu ndio ule uhabiki ninao waambia muuache jamani.

    ReplyDelete
  3. Unajisumbua brother.Hii blog imekuwa kama instagram group ya timu mojawapo.Fitina,majungu nä kukosa uweledi katika journalism ethics ndio sifa zake. Mimi nimeshafikia uamuzi enough is enough.

    ReplyDelete
  4. Mwanzoni nilidhani ni mzaha pale Yanga walipokuwa wanashangilia sare ya Simba.Jana tena kuna mashabiki wa Yanga walishangilia kwa furaha kutolewa nje ya mashindano na Mtibwa..Hivi kweli timu kubwa ya wananchi imefikia hapa.Hutokeaga ambalo unalifurahia ndiyo mwenyezi Mungu anakuzawadia!

    ReplyDelete
  5. Upuuzi ni hali anayokuwa nayo mtu anapoamua kufanya mambo ya kipuuzi. Hakuna timu ya kawaida inayofurahia sare kama hawana inferiority complex .Hali ya kuwa wewe ni duni au dhaifu kuliko mwenzako.Kushangilia kutolewa ni upuuzi wa hali ya juu au ni denial ya kukubali kutofanikiwa au kukubali hali yako ya udhalili na kukataa tamaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. More than inferiority complex,unajua mashabiki wa yanga wanaishi kwakudanganywa na uongozi yani wanachofanya nikujitia moyo kwamba wanaweza,ukichunguza
      yanga amepoteza mashabiki wengi sana katika kipindi hiki cha miaka miwili kama sio mitatu,ukweli ni kwamba uwezo hawana vidhibit vipo wazi ndio maana kama umeiangalia mechi ya simba na yanga utagundua mambo mengi sana yalikua yapo kishirikina zaidi na unyama wa nje nje,yanga kacheza faulu nying sana na hakukua na kadi zilizotolewa hili liko wazi kila mtu kaona,soka la bongo ni ujinga sana.

      Delete
    2. More than inferiority complex,unajua mashabiki wa yanga wanaishi kwakudanganywa na uongozi yani wanachofanya nikujitia moyo kwamba wanaweza,ukichunguza
      yanga amepoteza mashabiki wengi sana katika kipindi hiki cha miaka miwili kama sio mitatu,ukweli ni kwamba uwezo hawana vidhibit vipo wazi ndio maana kama umeiangalia mechi ya simba na yanga utagundua mambo mengi sana yalikua yapo kishirikina zaidi na unyama wa nje nje,yanga kacheza faulu nying sana na hakukua na kadi zilizotolewa hili liko wazi kila mtu kaona,soka la bongo ni ujinga sana.

      Delete
  6. Kwa hiyo kazawadiwa sare nyingine tena, ili aendelee kushangilia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic