AZAM FC kwa sasa wana uhakika wa kuendelea hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mlandege.
Bao hilo la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 59.
Leo Azam FC atamjua mpinzani wake ambaye atacheza naye kwenye hatua ya nusu fainali kati ya Simba ama Zimamoto.
Mshindi wa mchezo huu wa leo kati ya Simba na Zimamaoto atavaana na Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hili la Mapinduzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment