January 6, 2020


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana kufanya vema kwenye mashindano ya Mapinduzi ili kurejea na kombe lao ambalo walilitwaa msimu uliopita kwa kuifunga Simba kwenye fainali hizo kwa mabao 2-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wamejipanga kufanya kweli kwenye michuano hiyo itakayofanyika visiwani Zanzibar kuanzia leo, Januari 6,2020.
“Tunajua kwamba tuna kazi ngumu ya kufanya kwenye kombe la Mapinduzi ukizingatia sisi ni mabingwa watetezi tutapambana kulipata tena na kurudi nalo Tanzania, mashabiki watupe sapoti kwani tumejipanga vizuri,” amesema Maganga.
Azam FC ipo kundi A  ikiwa na Unguja, Yanga,Mlandege na Jamhuri itaanza kutetea taji lake leo, Januari 6 mbele ya Mlandege.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic