January 9, 2020


CHARLES Mkwassa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga leo atakuwa na kibarua mbele ya Mtibwa Sugar iliyo chini ya Zuber Katwila kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Amaan.

Timu zote mbili zimewahi kutwaa taji hilo mara moja ambapo Yanga ilitwaa taji hilo 2004 na Mtibwa 2010 leo zitamenyana kwnye hatua ya nusu fainali huku bingwa mtetezi akiwa ni Azam FC atakayecheza na Simba kesho, Januari 10, Uwanja wa Gombani.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Jamhuri huku Mtibwa Sugar ikipeta mbele ya Chipukizi kwa ushindi wa penalti 4-1 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic