WATANI wa jadi wanaongea kwa sana kutokana na kila mmoja kujivunia kikosi chake kipana na majembe ambayo wamefanya usajili kwa msimu huu kuelekea kwenye mechi yao itakayopigwa leo, Jumamosi, Januari 4, Uwanja wa Taifa.
Makocha nao wamekuwa wanawaamini wachezaji hao na wana rekodi zao walizoweka kwenye muda ambao wamecheza.
Mwisho wa ubishi itajulikana nani ni nani baada ya dakika 90 uwanja wa Taifa na utundu wao uwanjani kwa majembe hayo ya Simba na Yanga upo namna hii:-
Simba
Aishi Manula
Manula amecheza jumla ya mechi 12 ndani ya Simba sawa na dakika 1,080 akiwa langoni. Amefungwa mabao matatu na cleen sheet 9.
Alianza kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania, Simba 2-1 Mtibwa Sugar,Simba 3-0 Kagera Sugar, Biashara 0-Simba, Simba 1-0 Azam FC, Singida United 0-1 Simba, Mwadui 1-0 Simba, Simba 4-0 Mbeya City,Simba 0-0 Prisons, Simba 3-0 Ruvu Shoting, KMC 0-2 Simba, Simba 2-0 Ndanda.
Meddie Kagere
Ni kinara wa utupiaji akiwa ametupia jumla ya mabao 9 kwa sasa ndani ya ligi pia ametoa jumla ya pasi mbili za mabao ndani ya Simba.
Ameanza kwenye jumla ya mechi 12 ambazo ni sawa na dakika 1080. Msimu uliopita alifunga jumla ya mabao 23.
Mzamiru Yassin
Ameanza kwenye jumla ya mechi 10 ambazo ni sawa na dakika 900. Kwenye mechi alizoanza Yassin amekuwa ni mhimili ndani ya Simba ambapo ametoa jumla ya pasi tatu za mabao. Ni miongoni mwa wazawa ambao wanafanya vema kwa sasa ndani ya Simba.
Pascal Wawa-810
Beki kisiki ndani ya Simba, Pascal Wawa amecheza jumla ya dakika 810 ndani ya Simba. Kwenye mechi zote tisa aliazoanza ilikuwa ngumu ngome ya mlinda mlango wake kuguswa.
Hakucheza wakati Simba ikipoteza kwa mara ya kwanza mbele ya Mwadui FC kwa kufungwa bao 1-0, pia wakati Manula akitunguliwa na Edward Songo wa JKT Tanzania bao la kwanza pamoja na lile la pili alilofungwa na Mtibwa Sugar.
Miraji Athuman ‘Sheva’ -350
Alitumia dakika 30 mbele ya JKT Tanzania akichukua nafasi ya Deo Kanda na alifunga bao lake la kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-1 pia aliingia dakika ya 62 mbele ya Mtibwa Sugar akichukua nafasi ya Hassan Dilunga alifunga bao lake la pili na la ushindi wakati Simba ilishinda 2-1. Dhidi ya Kagera Sugar aliingia dakika ya 61 akichukua nafasi ya Deo Kanda.
Mbele ya Biashara United alitoka dakika ya 83 nafasi yake ilichukuliwa na Kanda alifunga bao lake la tatu.
Alimaliza dakika 90 mbele ya Singida United alifunga bao kwenye ushindi wa bao 1-0, Simba 4-0 Mbeya City, Ruvu Shooting 0-3 Simba alifunga mabao mawili na kumfanya afikishe jumla ya mabao sita ndani ya Simba na asisti moja akiwa amecheza jumla ya dakika 350
Molinga-899
David Molinga raia wa Congo maarufu kama mwili jumba ndiye amecheza mechi zote 11 na kutumia uwanjani dakika 899.
Ana mabao manne, alifunga mbele ya Polisi Tanzania mawili kwenye sare ya mabao 3-3, mbele ya JKT Tanzania Yanga ilishinda mabao 3-2 alifunga moja, zote uwanja wa Uhuru na bao la nne alifunga uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Alliance wakati Yanga ikishinda mabao 2-1.
Mechi nyingine alizocheza ni dhidi ya Ruvu Shooting1-0 Yanga1-0, Yanga 1-0 Coastal Union, Mbao 0-1 Yanga, Ndanda 0-1 Yanga,Yanga 1-1 KMC, Mbeya City 0-0, Yanga 1-0 Tanzania Prisons na Yanga 1-0 Biashara United.
Alifanyiwa mabadiliko kwenye jumla ya mechi tatu, mbele ya JKT Tanzania, dakika ya 60 nafasi yake ilichukuliwa na Abdulaziz Makame, Mbao Uwanja wa CCM Kirumba dakika ya 74 nafasi yake ilichukuliwa na Juma Balinya na mchezo wa Biashara United uwanja wa Taifa, dakika ya 45 nafasi yake ikachukuliwa na Tariq Seif.
Shikalo-720
Mlinda mlango namba moja wa Yanga, Farouk Shikalo amekaa langoni kwenye jumla ya mechi nane sawa na dakika 720. Amefungwa jumla ya mabao 5, clean sheet 4.
Ruvu Shooting 1-0 Yanga, Yanga 1-0 Coastal Union, Mbao 0-1 Yanga, Ndanda 0-1 Yanga, Yanga 3-2 JKT Tanzania,Alliance 1-2 Yanga, KMC 1-1 Yanga, Mbeya City 0-0 Yanga.
Sibomana
Mshambuliaji tegemeo ndani ya Yanga, Patrick Sibomana amecheza jumla ya mechi nane pia na ana mabao manne yote ameyafunga kwa mguu wa kushoto na ana pasi moja ya bao.
Deus Kaseke naye ameanza kwenye jumla ya mechi nane ana pasi tatu za mabao na beki kisiki Lamine Moro raia wa Ghana naye amecheza jumla ya mechi nane ndani ya kikosi cha Yanga
Tshishimbi- 676
Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi amecheza jumla ya mechi 9 ndani ya Yanga ambapo alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi saba huku mbili akitokea benchi.
Amecheza jumla ya dakika 676, mechi alianza wakati Yanga ikifungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting, Mbao 0-1 Yanga, Ndanda 0-1 Yanga, Yanga 3-2 JKT Tanzania, ,Mbeya City 0-0 Yanga, Yanga 1-1 KMC.
Alianzia benchi kwenye mechi dhidi ya Tanzania Prisons aliingia dakika ya 64 na kucheza dakika 26 akichukua nafasi ya Abdulaziz Makame, dhidi ya Biashara United dakika ya 70 na kucheza dakika 20 akichukua nafasi ya Mrisho Ngasa. Ndani ya dakika hizo 676 Tshishimbi ana asisti moja aliyotoa mbele ya Biashara United bao lilifungwa na Tariq Seif.
Juma Abdul-630
Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul amecheza jumla ya mechi 7 ndani ya Yanga ambazo ni sawa na dakika 630.
Mechi alizoanza ni dhidi ya Yanga 3-3 Polisi Tanzania, Yanga 1-0 Coastal Union, Mbao 0-1 Yanga, Ndanda 0-1 Yanga, Yanga 3-2 JKT Tanzania, Alliance 1-2 Yanga, KMC 1-1 Yanga.
Ana asisiti moja aliyotoa kwenye ushindi wa sare ya mabao 3-3 bao lilipachikwa kimiani na Mrisho Ngasa.
Abdulaziz Makame - 378
Kiungo Makame, amekuwa mwiba kwa wapinzani. Licha ya kutokuwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Tanzania Prisons aambapo alifanyiwa mabadiliko dakika ya 64 nafasi yake ilichukuiwa na Tshishimbi na Biashara United.Alifanyiwa mabadiliko kwenye mechi dhidi ya Mbao dakika ya 70 akichukua nafasi ya 76 na kucheza dakika 14, mechi dhidi ya JKT Tanzania aliingia dakika ya 60 akichukua nafasi ya David Molinga na kucheza dakika 30.
Ndani ya dakika Yanga 3-3 Polisi Tanzania, Yanga 1-0 Coastal Union alifunga bao lake la kwanza kwa kichwa, Yanga 1-0 Biashara United, kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons alitoka dakika ya 64 akiwa ametoa pasi moja ya bao kwa mpira wake wa kutupa akiwa nje ya uwanja, nafasi yake ilichukuliwa na Papy Tshishimbi.
Ameanzia benchi mechi dhidi ya Mbao aliingia dakika ya 74 akichukua nafasi ya Feisal Salim ‘Feitoto’, JKT Tanzania dakika ya 60 akichukua nafasi ya David Molinga.
0 COMMENTS:
Post a Comment