MAMBO yanazidi kuwa moto kwenye upande wa Ligi Kuu Bara ambapo kwa sasa vita ni ya wakongwe wawili ambao wanatarajia kuzima shughuli zote za Bongo kwa muda mchache kisha mambo mengine yataendelea.
Dakika 90 tu zinatosha kuweka heshima mpya ambao Simba itawakaribisha watani zao Yanga kwenye mechi ya ligi itakayochezwa uwanja wa Taifa.
Msimu ulipita wa mwaka 2018/19 Yanga iliambulia pointi moja tu kwenye sare ya bila kufungana ambapo shujaa wa mechi hiyo alikuwa ni Beno Kakolanya aliyeokoa michomo hatari ya Emanuel Okwi na Meddie Kagere ila ya mzunguko wa pili Kagere aliwatungua bao moja na kusepa na pointi tatu muhimu.
Vita kubwa itakuwa ni kwenye kuongeza rekodi ambazo wamejiwekea kwa sasa kwenye mechi zao ambazo wamezicheza na namba zo zipo namna hii kwa watani awa Simba na Yanga:-
Mechi walizocheza
Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vanderbrocek imecheza jumla ya mechi 13 ambazo ni sawa na dakika 1,170 huku Yanga iliyo chini ya Charlse Mkwasa imecheza jumla ya mechi sawa na dakika 990 za ligi.
Mechi za kushinda
Simba imeshinda jumla ya mechi 10 za ligi abazo ni dhidi ya JKT Tanzania ilifungwa mabao 3-1,Simba 2-1 Mtibwa Sugar, Kagera Sugar 0-3 Simba, Biashara United 0-2 Simba, Simba 1-0 Azam FC,Singida United 0-1 Simba, Simba 4-0 Mbeya City, Ruvu Shooting 0-3 Simba, Simba 4-0 Lipuli, KMC 0-2 Simba, Simba 2-0 Ndanda FC.
Yanga imeshinda jumla ya mechi 7 ambazo ni dhidi ya Coastal Union ambapo Yanga ilishinda bao 1-0. Mbao 0-1 Yanga, Ndanda 0-1 Yanga,Yanga 3-2 JKT Tanzania, Alliance 1-2 Yanga, Tanzania Prisons 0-1 Yanga, Yanga 1-0 Biashara United.
Kupoteza
Zote zimepoteza mechi moja Simba ilipoteza mbele ya Mwadui kwa kuchapa bao 1-0 huku Yanga ikipoteza mbele ya Ruvu Shooting na ilichawa bao 1-0.
Sare
Simba imelzimisha sare moja ya bila kufungana na Tanzania Prisons huku Yanga ikilazimisha sare tatu mbele ya Polisi Tanzania kwa kufungana mabao 3-3, Mbeya City ya bila kufungana na KMC 1-1.
Goal za kufunga
Simba imefunga jumla ya mabao 27 Yanga imefunga jumla ya mabao 14 huku muunganiko wa Molinga na Sibomana ukitupia jumla ya mabao nane na kwa kwani kila mmoja ametupia mabao manne na kwa upande wa Simba Kagere na Sheva wametupia jumla ya mabao 15 ambapo Kagere anayo tisa na Sheva sita.
Kinara wa kupachika mabao kwa Simba ni Meddie Kagere ametupia jumla ya mabao tisa na ana asisti mbili
Mkali wa pasi za mwisho
Francis Kahata kiungo mshambuliaji wa Simba ndiye kinara wa kutoa pasi za mwisho akiwa nazo nne huku kwa Yanga mwenye pasi za mwisho nyingi ni Deus Kaseke mwenye pasi tatu za mwisho.
Vinara wa mabao ya penalti
Idadi ya penalty ambazo Simba wamepiga mpaka sasa mpigaji wao akiwa ni Meddie Kagere aliyefunga mbili na Hassan Dilunga alifunga moja.
Penalti mbili alisababisha Miraj Athuman ilikuwa mbele ya Kagera Sugar wakati Simba ikishinda mabao 3-0 na mbele ya Mbeya City wakati Simba ikishinda mabao 4-0 na kwenye mchezo dhidi ya Lipuli Clatous Chama alikuwa chanzo cha penalti hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment