PASCAL Wawa,
beki kisiki wa Simba ni miongoni mwa wageni ambao wamekuwa na mchango mkubwa
ndani ya Simba baada ya kutua msimu uliopita wa 2018-19 akitokea nchini Ivory
Coast ambapo alishuhudia timu yake ikitwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa mara ya
pili mfululizo.
Kwa sasa
amekuwa na mhimili mhimili ndani ya Simba kwenye safu ya ushambuliaji
akishirikiana na Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Haruna Shamte, Keneddy Juma
kwenye ulinzi wa ngome yao wakiwa ndani ya uwanja.
Wawa
amecheza jumla ya mechi tisa kati ya 12ambazo imecheza Simba na alisimama imara
kwenye safu ya ulinzi kwani hakuruhusu wapinzani kuwaokotesha mipira nyuma ya
nyavu.
Mechi
alizoanza ilikuwa ni wakati wa Kocha Mkuu Patrick Aussems alimuamini kwenye jumla
ya mechi 7 nazo alikuwa imara muda wote ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar ikishinda
mabao 3-0 alikuwa ndani, Biashara United 0-2 Simba, Simba 1-0 Azam FC,Singida
United 0-1 Simba,Simba 4-0 Mbeya City, Simba 0-0 Tanzania Prisons, Ruvu
Shooting 0-3 Simba.
Hata sasa ameanza vizuri chini ya kocha mpya,
Sven Vanderbroek ambapo amecheza mechi mbili za ligi akianza kikosi cha kwanza
ilikuwa wakati Simba ikishinda mabao 4-0 Lipuli na KMC 0-2 Simba.
Mechi tatu,
Wawa hakuwa benchi kabisa ilikuwa ni mbele ya JKT Tanzania dhidi ya Simba iliposhinda mabao 3-1 Simba 2-1 Mtibwa Sugar pia na kichapo cha kwanza
kwa Simba msimu huu wa 2018-19 bao 1-0 ilichopokea Simba kwa Mwadui hakuwa
ndani ya uwanja wala benchi.
Januari 4, leo Jumamosi kutakuwa na pambano la kukata na shoka kati ya Simba na Yanga ambalo limeteka
hisia kubwa za mashabiki wa ndani na nje ya Bongo, Wawa anazungumza mengi
kuhusu ubora wake na hesabu kuelekea mchezo huo huyu hapa:-
“Wakati huu
wa sasa sio sawa na zamani, soka limekuwa na ushindani mkubwa na kila mmoja
anakiona kile unachokifanya jambo linalofanya kila wakati nipambane kujiweka
bora zaidi.
Unadhani
tofauti ya msimu huu na uliopita ni ipi?
“Kila muda
una changamoto zake kwa sasa hatuwezi kuzungumzia yale yaliyopita bali
tunatazama hapa ambapo tupo na kuona namna gani tunaweza kutoka.
“kila msimu
una ugumu wake na upekee jambo ambalo linafanya maisha ya soka yaendelee
kusonga mbele.
Unaipa
nafasi ipi timu yako ya Simba?
“Bado kwa
sasa ligi inaendelea kupata matokeo mwanzo haina maana kazi imesiha tuna
majukumu ya kuenelea kufanya zaidi ya hapa kwani kikubwa ambacho tunakihitaji
ni matokeo.
Kipi ambacho
kinawabeba kwa sasa?
“Ushirikiano
uliopo ndani ya Simba kila mchezaji pamoja na wale ambao wanatuongoza wanajua
namna ya kile ambacho tunahitaji kukifanya.
“Mashabiki
wanatupa sapoti katika kila jambo hiyo pia inaongeza nguvu yetu kufanya vizuri.
Ubora wako
umejificha kwenye nini?
“Kupenda
kile ambacho ninakifanya, kazi yangu ni kuona namna gani nafanya vema muda wote
hilo linanipa nguvu ya kuwa bora.
Mchezo wenu
dhidi ya Yanga unauzungumziaje?
“Hautakuwa
mchezo mwepesi kwani kila timu inahitaji ushindi, kwetu sisi kila baada ya
kumaliza mechi tunatazama mechi inayfuata hivyo hatuna presha yoyote na mechi
yoyote inayotuhusu.
Maandalizi
yapoje katika hilo?
“Tunafanya maandalizi
ya mechi zote hatujiaandai kwa ajili ya mechi dhidi ya Yanga pekee, kila timu
ambayo tunakutana nayo tunajiapanga ili kupata matokeo nina amini hata
wapinzani wetu wamejipanga kupata matokeo.
“Kama
ambavyo tunafaya siku zote tunalenga mbele zaidi hicho ndicho ambacho
tunakifikiria tunamaani tutafanya vizuri mashabiki watupe sapoti.
Unapata
picha gani ya mchezo huo?
“Kama ilivyo
mingine tu ni mchezo mzuri, tunawaheshimu wapinzani wetu. Kikubwa ni malengo na
kufanya kazi tukiwa timu hakuna kingine.
Unahofia
nini ukiwa uwanjani?
“Nikiwa
kwenye uwanja sina hofu yoyote zaidi ya kujifunza muda wote, ninaamini sitakuwa
bora endapo sitafanya makosa. Kupitia makosa najifunza kisha najifunza ili kuwa
bora.
Siri ya
mafanikio ni nini?
“Maombi kwa
Mungu, unajua yeye ndiye anayetufanya tunakuwa wajanja ndani ya uwanja, nje ya
uwanja na kwenye mambo mengine ambayo tunayafanya,”. Anamaliza Wawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment