NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa hana mashaka na mchezo wa leo mbele ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Amaan.
Simba itamenyana na Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi atakayefungwa leo anafungashiwa virago na kurejea Bongo na mshindi atamenyana na Mtibwa Sugar ambaye ameshakata tiketi yake jana, Januari 9, mbele ya Yanga.
"Ninatambua utakuwa mchezo mgumu ila hakuna cha kuhofia mbele ya Azam FC, tutapambana kufikia malengo yetu na tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Azam FC ina kumbukumbu ya kuitungua Simba mwaka 2019 mabao 2-1 kwenye mchezo wa hatua ya fainali, wanakutana leo wakiwa ni mabingwa watetezi na mshindi wa pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment