January 9, 2020


KESHO Simba itakuwa kazini ikimenyana na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi utakaochezwa Visiwani Zanzibar, Uwanja wa Amaan.

Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa ni wa kisasi kutokana na Simba kupotezwa mwaka 2019 kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 2-1.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck anatarajiwa kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa Kocha Mkuu wa Azam FC, Arstica Cioaba.

Simba ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Zimamoto na Azam FC ilishinda mbele ya Mlandege kwa bao 1-0 lililofungwa na Obrey Chirwa.

Kwa upande wa Simba, mabao yalifungwa na John Bocco ambaye ni nahodha, Sharaf Shiboub na Ibrahim Ajibu.

Simba imeongeza nguvu kwa kuwashusha majembe yake ya kazi ambayo yalibaki Dar ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere, Francis Kahata, Pascal Wawa na Meddie Kagere.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic