January 18, 2020


Imeelezwa kuwa wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM imewabana viongozi wa klabu hiyo katika suala zima la utoaji fedha kuhakikisha fedha zote wanakabidhi wenyewe na si kutoa kwa uongozi kutokana na kuhofia ‘kupigwa’.

GSM ambayo ilishinda tenda ya kuuza jezi za Yanga ikiwa ni pamoja na kuisaidia timu hiyo kiasi cha Sh mil 300 katika harambee iliyofanyika mwaka jana, imekuwa ikitoa mchango mkubwa ndani ya timu hiyo ikiwemo kusajili wachezaji na kumleta kocha Mbelgiji, Luc Eymael.

Wachezaji ambao wamesajiliwa chini ya GSM ni pamoja na Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Adeyum Saleh, Tariq Seif na Yipke Gislein ambapo fedha za wachezaji hao wamekabidhi wenyewe.

Taarifa ambazo Championi Ijumaa imezipata kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, licha ya GSM kuifanyia mambo makubwa timu hiyo likiwemo suala la usajili wa wachezaji na kocha, lakini wamekuwa makini katika suala la fedha kutokana na fedha zote kukabidhi wenyewe bila ya kuwahusisha viongozi.

“GSM wajanja sana, hawataki kupigwa kila kitu kinachoitwa fedha wanasimamia wenyewe na uongozi umekuwa ukishuhudia usajili tu na kukubaliana juu ya wachezaji na masuala mengine, lakini suala la fedha wamekuwa wakisimamia wenyewe.

“Hata suala la mishahara kwa sasa ipo chini yao na kocha pia imemlipa wao uongozi haukuhusika hata kidogo, nadhani wanafanya hivi ili kuepuka kuwekewa cha juu kwa maana ya kupigwa, hivyo ndiyo maana imeamua kumalizana wenyewe na wachezaji,” alisema mtoa taarifa huyo.

CHANZO: CHAMPIONI


4 COMMENTS:

  1. hawa inaonekana wakivunja mkataba wataaondoka na wahezaji wao

    ReplyDelete
  2. Naona mti upo hatari I kabla ya kutoa mauwa. Inaonesha wanaogopa yaliyowafika Simba. Ikiwa ni hivo nini itakuwa kazi ya uongozi ikiwa kila kitu wanaambuiwa? Tunawatakia watani kila la kheri

    ReplyDelete
  3. Hiyo inanyesha kiasi gani viongizi walivyo wajanja hadi hawaamiwi hata huko simba sina imani nako wachezaji wanasajiliwa kwa gharama uwanjani hamna kitu

    ReplyDelete
  4. Hii itasaidia kuondoa migogoro na wachezaji isiyokwisha juu ya maslahi yao kwa hilo hakuna ubaya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic