SVEN Vandrebroek, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake walicheza chini ya kiwango kipindi cha pili jambo lililofanya kuruhusu kufungwa mabao mawili kipindi cha pili licha ya wao kuanza kuifunga Yanga kwenye mechi iliyochezwa juzi uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Sven ambaye alikuwa akiingoza Simba kwa mara ya kwanza kwenye dabi ya Kariakoo na kushuhudia mabao mawili waliyoanza kuyafunga Simba yakipinduliwa na wapinzani wao Yanga ndani ya dakika saba za kipindi cha pili.
“Sijafurahishwa hata kidogo na tukio ambalo nimelishuhudia, kufungwa mabao mawili ndani ya dakika saba hili jambo ni baya na linaumiza, wachezaji hawajafanya kile ambacho nilitarajia mwanzo.
“Ninaamini kwamba walishindwa kujituma na kulinda ushindi waliopata kutokana na kujiamini kupita kiasi na kusahau kwamba mpira unaendelea, nitakaa na wachezaji wangu kuzungumza nao kwani hawajafanya vizuri kuruhusu mabao waliyoanza kufunga,” alisema Sven.
Ok sawa
ReplyDeleteYes hiyo ni sawa sawa manaake mchezo wa marudiano wapunguze magoli,duh ile timu ya wananchi sio mchezo
ReplyDeleteKweli ila nimewashangaa kushangilia droo wakati walikuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya goli 5.
DeleteAnatapatapa mara walikuwa pungufu
ReplyDelete