January 11, 2020


INAELEZWA kuwa Kiungo bora kwa msimu wa mwaka 2018/19 alipokuwa Simba, James Kotei yupo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Yanga ili ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria waliotwaa ubingwa mara 27.

Habari zinaeleza kuwa, Kotei ambaye alisepa Simba msimu wa 2018/19 baada ya kandarasi yake kumeguka na kujiunga na Kaizer Chiefs kwa sasa yupo kwenye hesabu za Yanga ili aongeze nguvu ndani ya kikosi hicho ambacho kimeanza kurejea kwenye kasi yake.

"Kotei yupo kwenye hesabu za kutua Yanga kwa sasa kutokana na uwezo wake mkubwa ambao anao, dirisha dogo wanajipanga kuongeza nguvu ukizingatia kuwa kocha mpya ameletwa," alieleza mtoa taarifa huyo.

11 COMMENTS:

  1. YANGA walimsaini Okwii pia mwisho wa siku? Kotei kama ameshindwa kupata namba South Africa basi ni mchezaji wa kiwango cha kawaida. Mchezaji ambae kwa Tanzania tunaweza kumuona babu kubwa ila timu zetu zinapoingia katika vita ya Africa kwa kuwategemea wachezaji bab kubwa mfano wa akina kotei ndipo tunapochemsha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu Lois Miquissone aliyesaini Simba mbona alikosa namba Sauzi au hii umeisahau?

      Delete
    2. Inawezekana uelewa wako ukawa mdogo kahata alikosa namba to mazembe kaja Simba kapata namba kiwaango kimepanda nasasa wamemwita kwakuwa ni Mali yao

      Delete
  2. Sasa unataka kulinganisha ligi ya South Africa na ya Tanzania? Ukilinganisha utakuwa unamatatizo kwenye uelewa wako

    ReplyDelete
  3. Na pia ligi ya Msumbiji siyo hata bora kama ya Kwetu. Kwa hiyo tuseme katoka Mozambique kuja huku basi hana ubora? Mtu akikosa namba sehem fulan haina maana siyo bora na akupata namba sehem fulan haina maana kuwa yuko imara inategemea na timu na ligi husika

    ReplyDelete
  4. Ila kwa kelele zote zinazopigwa juu ya usajili wa kotei ukweli unabaki ni mchezaji wa kawaida tu. Na ndio maana tunasema kama kotei kweli ni mchezaji wa daraja la juu kwanini ashindwe kuimudu ligi ya South Africa? Ligi yenye maslahi bora zaidi Africa. Anarudi Tanzania kwenye ligi inayochezwa kwenye vyombo vya habari zaidi kuliko viwanjani.

    ReplyDelete
  5. simba hadi baadhi ya mashabiki wake ni ugolo.
    kotri wakat yuko simba waliongea sana, leo anataka kujiunga yanga basi amsekuwa wa kawaida.
    huyu shabiki anatoa sababu nyepes sana.
    balinya mfungaji bora, lkn bongo kakosa namba.
    uwe na

    ReplyDelete
  6. Sasa linaua soka letu. Kotei anaondoka Simba akiwa ametangazwa kiungo bora wa timu. Kaondoka tukamsainisha Fraga ambae hafikii kiwango cha Kotei. Ukweli Simba haikumuongezea mkataba kwa kudanganywa kuwa mbrazil anaekuja anacheza kama Ngolo Kante. Mpaka anaondoka Simba Kitei alikuwa na kiwango kizuri. Leo roho zinatuuma na kumponda wa kawaida kwa kuwa jirani wamemtaka. Hii haina tofauti umeacha mke jamaa anampitia unaanza kusema alikuwa kikojozi. Kotei angekuwa wa kawaida tungemzawadia kiungo bora?????

    ReplyDelete

  7. Baadhi ya Mashabiki wa Kibongo hasa Simba, mchezaji akisajiliwa na upande wa pili Basi wanamshusha kiwango, yote kwasabab anaenda kwa mahasimu wao, ukiangalia hoja za Kumshusha kiwango Kotei haziingii akilini, Cha kushangaza wao pia wamwsajili mchezaji aliekua hachezi ktk kikosi cha Team yake S.A(Lois).
    Wakati mwingine Tupunguze ushabiki hata Kama Jambo hulipendi...

    ReplyDelete
  8. Huwezi kumfananisha Kotei na Fraga. Fraga ni next level. Mpaka anaondoka Simba kotei hajawahi kufunga hata bao la kuotea hata kwenye mazoezi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic